Follow by Email

Tuesday, July 24, 2012

Kumradhi Waziri Membe


Imeandikwa na Mhariri, Gazeti la Mwananchi (Tarehe 23 Julai, 2012)

Katika gazeti la tarehe 12/01/2011 tulichapisha habari yenye kichwa. Membe: Polisi walikiuka Maadili (Mabalozi waibana Serikali, wahoji polisi kutumia risasi za moto).

Habari hiyo ambayo ilifuatia tukio la vifo vya watu watatu na majeruhi kadhaa vilivyotokea mjini Arusha wakati polisi walipokabiliana na waandamanaji wa Chadema,  ilidai kwamba Waziri Membe alililaumu jeshi la polisi kwa kukiuka maadili, kuvuka mipaka yake na kusababisha mauaji hayo ambayo yalitia doa Tanzania.

Aidha habari hiyo iliendelea kudai kwamba mabalozi wa nchi mbalimbali walimbana wakitaka tamko la Serikali juu ya tukio hilo.

Baada ya uchunguzi wa kina, gazeti hili limebaini kuwa, Waziri Membe hakusema maneno hayo na wala hapakuwa na mvutano wala madai yeyote ya Mabalozi juu ya jambo hilo.

Kutokana na hayo, tunachukua fursa hii kumwomba radhi Waziri Membe, Jeshi la Polisi, Serikali, Mabalozi wote na Wananchi kwa ujumla.

Aidha tunapenda kumhakikishia Waziri Membe na wasomaji wote kwa ujumla kwamba habari hii iliandikwa kwa bahati mbaya na kwamba gazeti hili litaendelea kufanya kazi yake kwa kufuata misingi ya Taaluma ya uandishi wa habari, Maadili na sheria za nchi bila kumwonea mtu au kushinikizwa na mtu yoyote kwa maslahi binafsi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.