Follow by Email

Thursday, July 19, 2012

HAFLA YA KUMUAGA BALOZI WA HISPANIA‏

Balozi Rajabu Gamaha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akimkabidhi zawadi Mhe. Juan Manuel Gonzalez de Linares Palou, Balozi wa Hispania aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju (katikati) akiwa na baadhi ya Wageni waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo akiwemo  Mhe. Mhe. Alfonso Leinherdt (kulia) Balozi wa Marekani hapa nchini.

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu (wa kwanza kushoto) akiwa na baadhi ya Mabalozi walioalikwa kwenye hafla ya kumuaga Balozi Juan (wa kwanza kulia).


Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (kulia) akiwa na Mhe. Juan (katikati),  Balozi wa Hispania anayeondoka pamoja Mhe. Yudhistiranto Sungadi (kushoto), Balozi wa Indonesia hapa nchini katika hafla ya kumuaga Balozi Juan.Picha zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.