Follow by Email

Wednesday, April 18, 2012

Rais Kikwete akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tano nchini Brazil

   


Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia katika mkutano wa Open Government Partnership, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil tarehe 17 Aprili 2012.  


  
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu wa Georgie Mh Nika Gilauri katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil,baada ya kuhudhuria mkutano wa Open Government Partnership.  Wengine kwenye picha ni Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb) (wa tatu kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Ujumbe wa Tanzania ukibadilishana mawazo kabla ya ufunguzi wa mkutano wa Open Government Partnership uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil.  Kutoka kushoto ni Waziri katika Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. Mathias Chikawe, Waziri wa Kazi na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Mahadhi Juma Maalim na Mshauri wa Rais (Masuala ya Siasa) Dkt Laurian Ndumbaro.Ujumbe wa Tanzania, akiwemo Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Mshauri Mkuu Mwandamizi wa Rais katika masuala ya kidiplomasia, wakiwa kwenye mkutano wa Open Government Partnership katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil. Wajumbe wa Tanzania, akiwemo Bi. Grace Shangali (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Europe na America kwenye Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, pamoja na Wajumbe wengine kutoka taasisi mbalimbali za kiraia na serikali wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil,wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Open Government Partnership.


Picha zote na maelezo -   http://www.ikulublog.com/No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.