Follow by Email

Tuesday, April 24, 2012

Rais Kikwete ahudhuria mazishi ya Rais Bingu wa Mutharika nchini Malawi Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za rambirambi kwenye kaburi la aliyekuwa Rais wa Malawi, Prof. Bingu wa Mutharika


 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa Malawi marehemu Prof. Bingu wa Mutharika, kijijini Ndata, wilayani Thyolo, nje ya jiji la Blantyre, nchini Malawi jana.  Pembeni yake ni Mhe. Waziri Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.  


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa aliyekuwa Rais wa Malawi, marehemu Bingu wa Mutharika, Bi. Calista Mutharika wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini Ndata, katika mji wa Blantyre, Malawi tarehe 23 Aprili, 2012.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akionge na Rais wa Malawi, Bi. Joyce Banda, wakati wa mazishi ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Prof. Bingu wa Mutharika aliyefarika April 6 mwaka huu.  Mazishi hayo yalifanyika tarehe 23 Aprili, 2012 kijijini Ndata, wilayani Thyolo, katika mji wa Blantyre, Malawi.

Picha zote na:  FREDDY MARO, IKULU

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.