Follow by Email

Saturday, March 24, 2012

Taarifa kwa Watanzania wanaoishi nchini Mali


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kuwafahamisha Watanzania waliopo Mali kujiandikisha Wizarani kupitia email zifuatazo nje@foreign.go.tz au info@foreign.go.tz. Wakati wa kujiandisha tafadhali toa taarifa muhimu kuhusu Jina lako kamili, Umri wako,namba ya hati yako ya Kusafilia,mahali ulipo nchini Mali, simu yako pamoja na anuani ya barua pepe yako.

Aidha Wizara inapenda kuwashauri Watanzania popote walipo kutosafiri kwenda nchini Mali kutokana na kufungwa kwa mipaka ya nchi hiyo baada ya Kikundi cha Wanajeshi kupindua Serikali ya nchi hiyo na hivyo kusababisha Mipaka yote pamoja na Viwanja vya ndege.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.