Follow by Email

Friday, March 30, 2012

Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Nje yakutana na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje


Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) walipokutana na uongozi wa Wizara chini ya Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule, Katibu Mkuu wa Wizara na Balozi Rajab Gamaha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara.  Kamati hiyo ilikutana na uongozi wa Wizara kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kipindi cha kuanzia mwezi wa Januari hadi Machi mwaka huu 2012.Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2012.  Bw. John M. Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akieleza changamoto na mafanikio mbalimbali ya Wizara katika kipindi cha miezi Januari had Machi 2012.  Pichani ni Mhe. Mahadhi Juma Maalim (kulia), Naibu Waziri wa Wizara na Balozi Rajab Gamaha (kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara.


Makaimu Wakurugenzi wa Idara na Vitengo wakisikiliza taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara.


Makaimu Wakurugenzi wa Idara na Vitengo wakisikiliza taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara.Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Mhe. John Shibuda (Chadema-Maswa Magharibi) akichangia hoja.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.