Follow by Email

Wednesday, December 28, 2011

Naibu Waziri Mambo ya Nje Asaini Kitabu cha Maombolezo Leo Ubalozi wa Korea

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Mahadhi  J. Maalim akisalimiana na Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea leo jijini Dar es Salaam, alipofika kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Jenerali Kim Jong-Il.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Mahadhi J. Maalim akisaini Kitabu cha Maombolezo kwenye Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea leo jijini Dar es Salaam, kufuatia kifo cha aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Jenerali Kim Jong-Il.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Mahadhi J. Maalim akimfariji Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea Mhe. Kim Yong Su leo jijini Dar es Salaam, alipofika kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Jenerali Kim Jong-Il.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.