Follow by Email

Thursday, December 22, 2011

Naibu Waziri amuaga Balozi wa Zambia Nchini Tanzania


Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Mahadhi Juma Maalim akizungumza na Balozi wa Zambia nchini Tanzania Mhe. Mavis Muyunda alipofika ofisini kwake kumuaga leo tarehe 22.12.2011.

Balozi Mavis Muyanda akimkabidhi zawadi Mhe. Mahadhi Juma Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ofisini kwake leo kama ishara ya kumuaga. Balozi Muyanda anatarajiwa kuondoka nchini kesho tarehe 23.12.2011 baada ya kumaliza muda wake kazi nchini Tanzania.

Balozi Mavis Muyunda akiagana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Bi. Zuhura Bundala nje ya Jengo la Wizara alipofika kuagana na uongozi baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.