Follow by Email

Friday, November 11, 2011

Waziri Membe ahudhuria Tamasha la Vyuo Vikuu (Campus Night) FOCUS 11.11.11

Waziri Membe akisalimiana na Johannes na Maria Amritzer raia wa Marekani na wahisani wa tamasha la Usiku wa Vyuo Vikuu mara alipowasili viwanja vya Leaders Mjini Dar es salaam usiku wa Ijumaa tarehe 11.11.11

Waziri Membe akizindua kitabu cha FOCUS na Muandaaji wa Kongamano la Usiku wa Vyuo Vikuu Mchungaji Dkt. Huruma Nkone kwenye viwanja vya Leaders, Dar es salaam. 


Viongozi wa Victory Christian Centre waandaaji wa Tamasha la Usiku wa Vyuo Vikuu wakiimba wimbo wa Taifa na Waziri Membe wakati wa Ufunguzi wa Usiku huo.


Mass Choir ikitumbuiza kwenye jukwaa kuu

Umati wa Wanafunzi kutoka Vyuo mbalimbali wakishangilia wakati wa Tamasha la Usiku wa Vyuo Vikuu lililoandaliwa na Victory Christian Centre lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Waziri Membe akisoma risala kwenye tamasha la Usiku wa Vyuo Vikuu kwenye Viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam, tarehe 11.11.11


Waratibu wa tamasha hilo Harris Kapiga na Joseph Msami wakiwa kwenye picha na Waziri Membe mara baada ya kusoma hutuba yake. Kongamano hilo lilihudhuriwa na wanafunzi takriban elfu moja kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali nchini Tanzania.

Kikundi cha waimbaji wa Injili kutoka Sweeden kutoka kwenye shirika la SOS linalotoa huduma za injili duniani nao walikuwepo kutoa burudani kwenye tamasha hilo lililoshirikisha Vyuo mbalimbali nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.