Follow by Email

Tuesday, November 15, 2011

RAIS KIKWETE APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI WA UFARANSA NA USWISi IKULU JIJINI DAR LEO

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi mteule wa Ufaransa nchini Tanzania Mh Marcel Escure leo Ikulu jijini Dar es salaam.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi mteule wa Ufaransa Mh Marcel Escure baada ya kupokea hati zake za utambulisho leo Ikulu jijini Dar es salaamBaada ya Kupokea hati ya utambulisho

Rais Dkt Jakaya Kikwete akimtambulisha balozi mteule wa Uswisi nchini Tanzania Mh Oliver Chave kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Balozi Rajabu Gamaha ambaye anafuatiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani Bi. Grace Shangali na Mkurugenzi Msaidizi katika idara hiyo.

Rais Dkt Jakaya Kikwete akiongea na balozi mteule wa Uswisi nchini Tanzania Mh Oliver Chave baada ya kupokea hati ya utambulisho. Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.