Follow by Email

Wednesday, October 26, 2011

Mhe. Rais na Mama Kikwete wakutana na Jumuiya ya Watanzania waishio Perth Australia LeoRais Kikwete akihutubia Watanzania wanaoishi Perth Australia kwenye hafla fupi waliyomuandalia leo tarahe 26-10-2011

Rais Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa Mwekahazina wa Jumuiya Maryam Powell iliyotolewa na Watanzania hao kwa Rais kama ishara ya kumbukumbu ya mkutano huo. Walimshukuru Rais Kikwete kwa kuwatembelea na kuahidi kuleta fursa mbalimbali haswa za uwekezaji ili kuendeleza uchumi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bwana John Haule akisalimiana na Mahir Meghji, Mtanzania anayeishi Perth Australia. Ujumbe wa Watanzania uko Mjini Perth kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola.

Balozi wa Tanzania Nchini Japan na Australia Mhe. Salome Sijaona akisalimiana na mwakilishi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Australia.

Katibu wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Perth Australia Pendo Mwaiteleke (wa pili kulia) akiwakaribisha wageni kumsikiliza Rais Kikwete kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na Jumuiya hiyo leo Mjini Perth Australia.

Baadhi ya Wabunge na Waziri walioongozana na msafara wa Mhe. Rais Kikwete kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola

Baadhi ya Watanzania na marafiki wa Tanzania waliohudhuria hafla hiyo.

Wana habari walioongozana na msafara wa Rais Kikwete Anna Nkinda (maelezo) na Jaffar Haniu (TBC) nao hawakuwa nyuma kuhakikisha wanapata matukio yote muhimu ya hafla hiyo.

Mama Salma Kikwete akiwa na baadhi ya Watanzania waliohudhuria hafla hiyo.

Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na Wanajumuiya kwenye picha ya pamoja na viongozi wao

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.